28 Januari 2013 - 20:14

Rais wa Afghanistan Haamid Karzay kukutana na mjumbe rasmi wa Marekani Afghsnistan, Sherehe za wiki ya umoja Afghanistan, Miripuko katika misafara ya kijeshi na kuondoka mtoto wa malikia Afghanistan ni miongoni mwa habari za picha za wiki ilopita.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA-  Haamid Karzay rais wa Jamuhuri ya Afghanistan katika maongezi yake na mjumbe rasmi wa Marekani alieleza kua Marekani lazima ifuate na kufanyia kazi mikataba na makubaliano baina ya Kabul na Washington katika mambo ya  Afghanistan na Pakistan.

Maongezi hayo yalifanyika katika Ikulu ya Afghanistan na kudurusu maongezi ya suluhu ya Marekani na Taleban katika nchi ya Qatar.

Mtoto wa Malikia ambae ni mtoto wa mrithi wa malikia wa Uingereza (Herri) aondoka Afghanistan baada ya opresheni za kijeshi zilodumu kwa muda wa miezi 5 arejea Uingereza.

Baada ya uvamizi wa msafara wa kijeshi mashariki mwa Afghanistan watu wasopungua 5 kuaga dunia na 15 kujeruhiwa vibaya.

Kwa munasaba wa maulid ya Mtume Muhammad(saw) na wiki ya umoja, Waislamu wote katika kila sehemu ya Afghanistan kusheherekea siku adhimu hiyo.

Kijana wa Kiafghanistan pamoja ya kuwa na ulemavu wa kidhahiri aonyesha hisia yake ya ndani ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu na uhusiano wake na Mola wa viumbe.